Jumapili 24 Agosti 2025 - 00:42
Haya ndiyo makundi matano mabayo hayatapata shafa'a (Uombezi siku ya kiyama)

Hawza / Riwaya za Kiislamu hazijaihesabu shafa'a kwenye makundi matano: makafiri, washirikina, wanafiki, wakanushaji wa shafa'a, na wale wanaoibeza Swala. Imam Swadiq (a.s) kwa msisitizo alisema kuwa hata katika nyakati za mwisho za maisha yake, shafa'a ya Ahlul-Bayt kamwe haitamfikia mwenye kuipuuza Swala, hili linaonyesha kwamba kutoijali Swala ndio kizuizi kikubwa zaidi cha kunufaika na shafa'a

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Nāsir Rafii katika moja ya hotuba zake alizungumzia mada ya “kutopata shafa'a makundi matano maalumu Siku ya Kiyama”, ambayo tunaiwasilisha kwenu kama ifuatavyo:

Riwaya za Kiislamu zinaeleza kwamba shafa'a haijumuishi makundi haya matano, na watu hawa wako nje ya upeo wa shafa'a.

Kundi la kwanza ni makafiri; kwa mfano, katika vyanzo imeelezwa kwamba watu kama Abu Jahl, kamwe hawatapata shafa'a.

Kundi la pili ni washirikina; wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wawe wanaamini miungu wawili, watatu, au zaidi.

Kundi la tatu ni wanafiki; Katika mafundisho ya dini imeelezwa kwa msisitizo kwamba unafiki ni mbaya zaidi kuliko ukafiri, kwa sababu mnafiki kwa dhahiri hujionyesha kuwa muuminj lakini kwa ndani huamini na hutenda kinyume.

Kundi la nne ni wakanushaji wa shafa'a; wale wanaokataa kabisa kuwepo kwa shafa'a na kuiona kuwa ni kitu kilicho tengenezwa na wa wanazuoni, ni wazi kwamba mtu asiyeliamini jambo la asili la shafa'a, hawezi kamwe kustahiki shafa'a.

Kundi la tano ni wale wenye kuidharau Swala na hawatoi umuhimu unaostahiki kwenye ibada hii tukufu: Imepokewa katika riwaya kwamba Imam Swadiq (a.s) alisema: “Shafa'a yangu kwa yule anayeibeza Swala na kuiona haina thamani, kamwe haitamfikia.” Kubeza huku kunaweza kujitokeza kwa namna mbalimbali; wakati mwingine mtu huichelewesha Swala ili kwanza ashughulikie mambo mengine, kama vile kutazama filamu, kufuatilia mechi ya mpira, kula matunda au kupumzika, katika hali kama hiyo, Swala haimo katika kipaumbele, na kwa vitendo inaonekana haina umuhimu, imenukuliwa kwamba baadhi ya watu huswali Sala ya Alfajiri kwa mtindo uitwao “Midomo ya Dhahabu” (لب طلایی); yaani pale jua linapokuwa linapanda, ndipo humaliza kusali Alfajiri.

Vivyo hivyo, Swala ya Magharibi mara nyingine hucheleweshwa hadi dakika za mwisho za “Ukingo wa Dhahabu” (حاشیه طلایی) wa machweo; yaani jua likiwa linakaribia kutua kabisa ndipo mtu anapokumbuka Swala, tabia hii inaonyesha kwamba mtu ameweka Swala pembezoni mwa maisha yake, na siyo katika msingi wa maisha yake ya kidini, katika riwaya muhimu sana imesimuliwa kwamba Imam Swadiq (a.s), katika nyakati za mwisho za maisha yake matukufu, alipokuwa katika kitanda cha mauti, alisema: “Wakusanyeni ndugu zangu wa karibu,” Mke wake anasema: “Tuliwajulisha wote wana familia na tukawakusanya, kwa kuwa tulidhani kwamba anataka kusema neno muhimu sana na lenye athari kubwa.”
Baada ya wote kuhudhuria, Imam Swadiq (a.s) kwa uwazi alisema: “Tambueni kwamba shafa'a yetu kwa yule anayeibeza Swala na kuiona duni, kamwe haitamfikia.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha